HASO ZA VIJANA cover art

Letras

[Intro]
Jboy on the mic
Eeh
Vijana twende kazi sasa
Haso za vijana
Haso za vijana

[Verse 1]
Maisha yetu sisi vijana tuna haso
Leo ndoto nyingi
Kesho hata nauli hatuna boss
Tunacheka mchana
Usiku mawazo yanatutesa
Lakini bado tunasimama
Hatutaki kuonekana wanyonge kabisa
Mfukoni hakuna kitu
Moyo una matumaini
Marafiki wanageuka
Wanapoona hali ni ngumu kweli
Lakini kijana ni chuma
Hatakubali kushindwa
Anaanguka mara nyingi
Lakini bado ana-inuka tena

[Chorus]
Haso za vijana
Tuna-beba bila kulia
Tuna-kimbiza siku
Hadi jasho liwe maji
Hata kama leo ni ngumu
Kesho tuta-tulia
Haso za vijana
Hadi tufike mbali

Haso za vijana
Tuna-sema tumechoka
Lakini roho haitoi
Bado ina-nipush mbele
Kila kona mtaa
Ndoto zinatembea
Haso za vijana
Mpaka tume-fika ndege

[Verse 2]
Asubuhi foleni
Jioni tunafunga duka
Mama anauliza
“leo mmeuza nini huko?”
Tunabana mia
Mia
Tukitafuta njia
Tunaandika mipango kwenye karatasi ya sukari
Madem wanataka soft life
Sisi bado tupo ground
Tunavaa suruali moja wiki nzima round
Lakini tume-apa
Familia haitabaki hivi
Kesho tukifanikiwa
Wote wanacheka rasmi

[Chorus]